UNYAMA HUU HADI LINI?
Wakati sakata la kifo Cha binti yetu wa singida Nusura Abdalla wa chuo Cha UDOM likiendelea Kwa kufanyika uchunguzi dhidi ya kifo chake , tumepata pigo lingine Kwa mwana singida mwenzetu Dkt. Isack Daniel Athuman Sima kukatwa mapanga na watu wasiofahamika huko wilayani Tarime akitoka kazini kwake kituo Cha afya Nyantongo .
Dr. Isack Daniel Sima aliajiriwa sekta ya afya mnamo mwaka 2020 kupitia ajira za madaktari 1000 na alipangwa kituo Cha kazi huko Tarime mkoa wa Mara . Wahalifu wamekatisha uhai wa ndugu yetu ambaye alikuwa ni nguvu kazi Kwa taifa na familia yake . Matukio haya ni mabaya hivyo ni muhimu uchunguzi wa kina ufanyike ili kuwabaini wahalifu waliohusika na mauaji haya ili wafikishwe mbele ya vyombo vya sheria wapate haki yao. Pumzika Kwa Amani IsackDaniel Sima.
Sehemu kama hizi serikali inabidi wapeleke wafanyakazi wa kijeshi ili waende kijeshi heshima itakuja maana democracy hawaitaki
Maoni
Chapisha Maoni