MIRADI YA MAENDELEO IRAMBA
RC. SERUKAMBA ATEMBELEA NA KUKAGUA MIRADI YA MAENDELEO ZAIDI YA 30 INAYOTEKELEZWA KATIKA HALMASHAURI YA IRAMBA
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba Mkoani Singida Gunna Maziku.ameagizwa ,Kuhakikisha anakutana na wakuu wa idara na kupanga namna ya kusimamia na kuelekeza nguvu zaidi kwenye miradi inayosuasua, Ili Kuhakikisha ifikapo Juni 30 Miradi hiyo iwe imekamilika.
Agizo hilo limetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Singida, Peter Joseph Serukamba baada ya Kutembelea na Kukagua miradi ya Maendeleo zaidi ya 30 inayotekelezwa Wilayani humo.Mei 16 na 17 Mwaka huu.
RC Serukamba amewahimiza Viongozi na wasimamizi wa miradi hiyo kuhakikisha wanakamilisha miradi hiyo kwa wakati uliopangwa na hasa kabla ya Juni 30 Mwaka huu.
Katika miradi ambayo, Inahitajika kumalizika haraka kwa lengo la kutorudishwa kwa fedha za serikali kabla ya Mwaka Mpya wa Fedha kuanza ni pamoja na miradi ya Shule Mpya zinazojengwa ambazo ni za Mradi wa BOOST hasa kwa Shule za Msingi kwa lengo la Kuhakikisha watoto wote wamepata haki ya kusoma na kuondoa mdondoko wa KKK 3 yaani kusoma,kuandika na kuhesabu.
Serukamba akiwa katika ziara yake Wilayani Iramba amekagua miradi ya ujenziwa Barabara na madaraja , Amekagua Zahanati, Matundu ya vyoo katika Zahanati, Matundu ya vyoo vya Shule za Sekondari na Msingi, Madarasa kwa Shule za Msingi, Mabweni kwa Shule za Sekondari, Bwalo la chakula kwa Shule za Sekondari pamoja na Kituo cha Walimu cha TRC.
Aidha miradi hiyo mpaka ikamilike inatarajia kutumia zaidi ya Shilingi za Kitanzania Bilioni 8.8 ambapo mpaka sasa zimetumika zaidi ya Shilingi Bilioni 4.2 na bado miradi hiyo inaendelea kutekelezwa kulingana na Matakwa ya serikali.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba Gunna Maziku, yeye kwa upande wake amesema kuwa, wao kama Halmashauri watahakikisha wanasimamia kwa ufanisi mkubwa miradi hiyo na Kuhakikisha imekamilika kwa wakati; hasa Juni 10 hadi Juni 20 Mwaka huu.
Maoni
Chapisha Maoni