ZUIA UFISADI KWA MAENDELEO YA TAIFA
Ndugu zangu habari. Mimi Frank Henry Magili Joseph Ikululyabopye, nimeandika kitabu ambacho kitakuwa ndiyo mwarobaini/suluhisho la kudumu la kuutokomeza Kabisa UFISADI. Katika kitabu hiki Chenye kichwa cha habari "JINSI YA KUSHUGHULIKIA UFISADI KWA MAENDELEO YA TAIFA LETU" Nimeandika historic ya UFISADI katika Taifa let, tangu serikali ya awamu ya kwanza iliyoongozwa na hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere had serikali ya awamu ya Tano chini ya MHE.Rais Dr. John Pombe Joseph Magufuli. Nimeangalia jitihada za serikali za kupambana na UFISADI na jinsi ambavyo UFISADI umekuwa ukiibuka kwa sitaili ya aina yake. Pamoja na mambo mengine nimegusia ni nini hasa kinawafanya watu wajiingize kwenye vitendo vya UFISADI. Kikubwa Karisa katika kitabu ni lile suluhisho la kudumu nililolitoa la jinsi gani ya kukabiliana na UFISADI na hatimaye kuutokomeza Kabisa. Mwandishi ameona kuwa UFISADI ni dhana tata, hivyo vita yake pia ni tata. Hii ni kutokana na ukweli kuwa UFISADI hauna sura hubadirikabadirika kama kinyonga kulingana na mazingira pamoja na wakati uliopo. Na huwa unafanyakazi katika mikono iliyofichika. Kwakuwa vita yake ni tata hivyo basi na silaha zake zinatakiwa ziwe za aina tofautitofauti zenye sifa mbalimbali kama vile uwezo wa kutoa mashambulizi ya karibu, ya Kati na ya mbali kabisa. Hivyo basi mwandishi amebainisha kuwa vita dhidi ya UFISADI ni vita ya pamoja kutoka ngazi ya mtu mmoja mmoja hadi ngazi ya kitaasisi. Mwisho : Ningependa kitabu hiki kimfikie kila mtanzania popote alipo iwe mjini au vijijini jipatia kopi yako moja kwa bei ya Tshs10,000/= wasiliana kwa namba ya simu 0764-759060. Vilevile kwa watu ambao hupata fursa ya kuandaa makongamano mbalimbali, mikutano mbalimbali iwe ya kisiasa au ya kitaaluma n. k usisite kunialika na kunipatia dakika 5-10. Iliniweze kuelezea Dhana ya UFISADI na jinsi ya kuutokomeza kwa maendeleo ya Taifa letu.Huduma hii itakolewa bure. Usisite kusambaza ujumbe huu kwenye magroup mengine kwa usitawi wa Taifa letu ni mimi Frank H. M. J. Ikululyabopye (PhD in Finance-student).
Ni kitabu kizuri sana na ninapendekeza kitumike kwenye mashule kama kitabu cha ziada
JibuFutaAsante kwa maoni yako
Futa