MATUMAINI YAANZA KUREJEA YANGA
Wachezaji Youthe Rostand, Juma Abdul, Haji Mwinyi, Andrew Vicent, Pato Ngonyani,Thabani Kamusoko na Ibrahim Ajib wako tayari kurejea kikosini kama benchi la ufundi litaona inafaa.
Daktari wa Yanga Dk Edward Bavu ameuambia mtandao rasmi wa Yangakuwa idadi ya wachezaji majeruhi sasa imepungua kutoka 11 na kubaki wanne tu.
"Rostand,Juma Abdul,Hadji Mwinyi, Andrew Vicent,Pato Ngonyani,Thabani Kamusoko,Ibrahim Ajib wote hawa wako tayari kwa kurejea uwanjani.
"Hii ina maana kuwa wataalamu wetu wa ufundi wanaweza kuwatumia endapo wataoana inafaa kufanya hivyo kulingana na mazoezi waliyowapa, wakati mwingine mchezaji kucheza inahitaji utimamu wa asilimia mia moja," amesema Dk Bavu
Kurejea kwa wachezaji hao kunazidi kuimarisha kikosi cha Yanga ambacho kesho kinashuka kwenye uwanja wa Taifa kuumana na St Louis ya Shelisheli.

Maoni
Chapisha Maoni