KUREKEBISHA MZUNGUKO WA HEDHI

AFYA / MATATIZO YA KINA MAMA2

Kurekebisha mzunguko wa hedhi

BY EJM

Kurekebisha mzunguko wa hedhi

Tatizo la kuvurugika kwa mzunguko wa hedhi huanza ghafla au polepole ambapo mwanzo mwanamke alikuwa akipata siku zake katika utaratibu unaoeleweka lakini mara haelewi au hajielewi namna mzunguko wake unavyoenda.

Kuvurugika kwa hedhi ni kitendo cha mwanamke kuanza kuona siku zake bila tarehe au mzunguko maalumu na matokeo yake ni kuwa mwanamke atashindwa kutimiza malengo yake kwa kutumia mzunguko huo sababu ni haueleweki.

Unaweza kutokewa ghafla tu unapata hedhi mahali usipotarajia jambo linakufanya ubaki na woga na huelewi nini cha kufanya kwani hukuwa umejiandaa kwa tukio hilo kama matokeo ya siku zako kutokuwa mzunguko maalumu. Wakati mwingine unaweza kupitiliza mwezi hata miezi kadhaa bila kuona kabisa siku zako na hata ukipima ujauzito unakutwa huna ujauzito wala dalili huna.

Madhara ya kuvurugika kwa mzunguko ni pamoja na;  kushindwa kupata ujauzito, maambukizi katika kizazi na kuziba kwa mirija ya uzazi.

Kwanini unahitaji mzunguko wa hedhi ulio sawa?

Faida za kuwa na mzunguko wa hedhi ulio sawa:

Utakusaidia kupata ujaouzito ulioupangiliaUtakuepusha kupata ujauzito ambao hukuupangiliaUtaweza kuamua jinsia ya mtoto unayemtaka

Nini husababisha kuvurugika kwa mzunguko wa hedhi

Ni rahisi kugundua kama mzunguko wako umevurugika ikiwa tu unauafahamu vizuri mzunguko wako ulio sahihi. Kufahamu mzunguko unahitaji uifahamu siku ambayo ulianza kuona damu hadi siku utakapoona tena katika mzunguko unaofuata. Karibu kila mwanamke huwa na mzunguko wake usiofanana na wa mwingine.

Tatizo linaweza kuanza kwa kurukaruka siku, mwanamke pia anaweza kupoteza siku yaani mwezi mwingine anaona na mwezi mwingine haoni, au anaingia mara mbili kwa mwezi au anaona damu ya hedhi kwa siku nyingi hata zaidi ya siku arobaini mfululizo. Damu yake inaweza kutokea kidogo kidogo ikiwa na mabonge mabonge.

Zifuatazo: ni  sababu za hedhi kubadilika:
  1. Mabadiliko ya mazingira ambayo hupelekea mfumo wa mwili hubadilika pia hasa mwanamke akitoka sehemu ya joto kwenda mikoa ya baridi au toka mikoa ya baridi kwenda mikoa ya joto.
  2. Msongo wa mawazo (stress)
  3. Hofu
  4. Woga
  5. Mabadiliko ya kisikolojia
  6. Uvimbe kwenye kizazi
  7. Matatizo kwenye mfumo wa homoni
  8. Matatizo kwenye vifuko vya mayai
  9. Mimba kuharibika
  10. Maambukizi sugu ya kizazi pia ni mojawapo ya sababu.
  11. Maumivu ya tumbo chini ya kitovu ya mara kwa mara na kila ukipima unaambiwa ni ugonjwa wa U.T.I kumbe siyo yutiai
  12. Kutokwa na uchafu ukeni
  13. Maumivu wakati wa tendo la ndoa

Maoni

Machapisho Maarufu