CHRISTIAN RONALDO ATOA SOMO KWA WACHEZAJI
*KUNA BINADAMU WA AJABU SANA DUNIANI!!!*
CHRISTIANO RONALDO, Mchezaji bora kabisa duniani aliwashangaza wengi alipomshukuru rafiki yake wa utotoni ALBERTO FANTRAU wakati akipokea tuzo yake-"Ndio, mimi ndiye mchezaji bora duniani lakini mafanikio yangu yote ni kutokana na rafiki yangu mkubwa ALBERTO FANTRAU, asante sana FANTRAU".
Wengi walistaajabu na kujiuliza FANTRAU ni nani?
RONALDO akasimulia:
" Mimi na FANTRAU tulicheza timu moja tukiwa watoto. Siku moja mascout wa Sporting Lisbon walikuja kutafuta vipaji eneo letu. Kabla ya kuanza mchujo walituambia kuwa mchezaji atakayefunga magoli mengi zaidi tutampeleka Academy ya Sporting Lisbon".
"Siku hiyo timu yetu ilishinda 3-0. Mimi nilifunga goli la kwanza na FANTRAU akafunga la pili."
" Goli la tatu ndilo lenye historia ya ajabu. FANTRAU alipata mpira na kubaki na kipa kisha akampiga chenga na kubaki na wavu tu mimi nikiwa pembeni yake. FANTRAU angeweza kufunga yeye lakini kwa mshangao wa kila mtu akaamua kunipasia mimi na nikafunga."
"Mimi mwenyewe nilishangaa sana na baada ya mechi nikamfuata FANTRAU na kumuuluza -"kwanini hukufunga wewe ili uchukuliwe na Sporting Lisbon Academy?" Nae akajibu-"Niliamua kukupasia wewe ufunge kwasababu naamini wewe ni bora kuliko mimi".
Hivyo, RONALDO alipata nafasi Academy hiyo lakini FANTRAU hakucheza tena mpira. Hata hivyo, toka wakati huo RONALDO hajamsahau hata kidogo FANTRAU kwani bila yeye huenda asingepata mafanikio hayo. RONALDO amemfanya FANTRAU kuishi maisha mazuri na FANTRAU hakosi kuhudhuria mechi zote za RONALDO na RONALDO mara nyingi hushangilia magoli yake na FANTRAU.
MAFUNZO:
1. Mpende jirani yako
2. Hata ukifanikiwa usisahau ulikotoka

Maoni
Chapisha Maoni